Mfumo wa hatimiliki wa Torrens

Mfumu wa hatimiliki wa Torrens ni mfumo unaotumika kusajili hatimiliki ya ardhi ambapo serikali inawajibika na kuwahakikishia wale wamejumuishwa katika rejista cheti cha hatimiliki cha ardhi ambacho hakiwezi kupingwa kivyovyote. Mfumo huu uliaandaliwa kukabiliana na matatizo ya kutokuwa na uhakika, utata na gharama iliyohusikana na mfumo wa zamani wa hatimiliki, ambao ulitegemea ushahidi wa hatimiliki wa hapo mbeleni usikuwa na dosari hadi kwenye muanzilishishi wa umiliki.

Mfumo wa hatimiliki wa Torrens ulianzishwa katika Australia Kusini mwaka 1858, na uliandaliwa na aliyekuwa mkuu wa serikali ya kikoloni wa Australia Kusini, Sir Robert Torrens. Tangu hapo, umekubalika kwenye Mataifa ya Jumuiya ya Madola ui na umeenea sana duniani kote.

Nchini Marekani, majimbo yanayo zingatia utekelezaji japo kwa kiwango kidogo wa mfumo huu ni Minnesota, Massachusetts, Colorado, Georgia, Hawaii, New York, North Carolina, Ohio, na Washington.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search